pmbet

Trump asema ni 'siku ya ukombozi', atangaza ushuru mkubwa duniani

Eric Buyanza

April 3, 2025
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza ushuru mkubwa kwa mataifa mbalimbali katika kile alichokiita "siku ya ukombozi", na hivyo kuzidisha hofu ya kutokea kwa vita vya kibiashara duniani.

Washirika mbalimbali wa Marekani wameguswa na hatua hiyo. Nchi za Umoja wa Ulaya zimewekewa ushuru wa asilimia 20 kwa bidhaa inazouza nchini Marekani, huku China ikiwekewa asilimia 34 na nchi ya kusini mwa Afrika ya Lesotho ikiwekewa kiwango cha ushuru wa asilimia 50.

Mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uingereza, Brazil, Mexico, Australia, Uswisi, Poland na mengineyo yamekosoa hatua hiyo ya Trump huku baadhi yakisema si ishara ya urafiki na yako tayari pia kujibu mapigo. Hata hivyo  utawala wa Trump umesema hautaitoza ushuru wowote mpya Urusi kwa sababu biashara kati ya nchi hizo mbili imepungua maradufu kutokana na vikwazo vya Marekani tangu Moscow ilipoivamia Ukraine.

Mapema mwaka huu, Trump aliwaagiza maafisa wake kuandaa mpango wa kile kiitwacho "ushuru wa malipizano" kwa bidhaa zinazoingia Marekani, akitekeleza ahadi yake ya kampeni "ya jicho kwa jicho" kwenye masuala ya biashara ya kilimwengu.

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet