Trump asema Urusi imeapa kulipa kisasi kwa Ukraine
Eric Buyanza
June 5, 2025
Share :
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amezungumza kwa mara nyingine tena na Rais Vladimir Putin wa Urusi na kutahadharisha kwamba usitishwaji wa vita nchini Ukraine hauwezi kufikiwa katika siku za karibuni.
Trump amesema kiongozi huyo wa Urusi ameapa kulipiza kisasi baada ya Ukraine kushambulia ndege zake za kivita zipatazo 40.
Trump amesema kupitia mtandao wake wa kijamii ya Truth kwamba ingawa yalikuwa mazungumzo mazuri, lakini bado hayafungui njia ya kupatikana amani ya haraka.
Mazungumzo yao yamefanyika siku tatu baada ya Ukraine kushambulia kambi za kijeshi za Urusi, ikisema imeharibu ndege za thamani ya mabilioni ya dola.
DW