Trump ataka kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya Ukraine
Eric Buyanza
March 20, 2025
Share :
Ikulu ya White House imesema kwamba umiliki wa Marekani wa vinu vya nyuklia vya Ukraine ulijadiliwa wakati wa simu ya siku ya Jumatano kati ya Trump na Zelensky - ingawa rais wa Ukraine baadaye amesema pendekezo hilo lilitolewa tu kuhusu kituo cha Zaporizhzhia kinachoshikiliwa na Urusi.
Kufuatia mawasiliano kati ya marais hao wawili, mwanadiplomasia mkuu wa Washington Marco Rubio alisema "umiliki wa Marekani wa mitambo hiyo itakuwa ulinzi bora kwa miundombinu hiyo na msaada kwa miundombinu ya nishati ya Ukraine".
Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, kusini mwa Ukraine, ndicho kikubwa zaidi barani Ulaya.
Vikosi vya Urusi vilikiteka kinu hicho muda mfupi baada ya kuanzisha uvamizi wao kamili wa Februari 2022 na wamekikalia tangu wakati huo, pamoja na eneo kubwa la Zaporizhzhia.