Trump atishia kuiangamiza Iran, iwapo watajaribu kumuua
Eric Buyanza
July 11, 2026
Share :

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya serikali ya Iran kwamba Marekani itafanya mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya Iran ikiwa itachukua hatua yoyote ya kuhatarisha maisha yake au kujaribu kumuua.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump aliandika, “Makombora elfu moja yako tayari na yameelekezwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ikiwa tishio la serikali ya Iran la kumuua Rais wa Marekani litatekelezwa, makombora zaidi ya elfu moja yatafyatuliwa mara moja.”
Trump pia alisema kuwa ametoa maagizo yanayohitajika na kwamba jeshi la Marekani liko tayari "kuangamiza kabisa maeneo yote ya Iran" kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kauli ya Trump inajiri kufuatia ripoti za ujasusi kutoka Israel zinazodai kuwepo kwa njama mpya ya Iran ya kutaka kumuua Trump, pamoja na picha na mabango zilizoonekana wakati wa mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei.
Maafisa wa Iran wamekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa kumuua Trump.
BBC





