pmbet

Trump atoa ramani ya Hormuz na kuipatia jina 'Strait of Trump'

Eric Buyanza

April 30, 2026
Share :

Rais Donald Trump amechapisha ramani ya Mlango-Bahari wa Hormuz kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, Truth Social, baada ya kuuita jina la "Strait of Trump ".
 

Trump amewahi kuetumia neno "Trump Strait" wakati wa hotuba, na kusema kwa mzaha kwamba vyombo vya habarivinaweza kufikiria kuwa ni "kosa la kukusudia," lakini kila mtu anajua sio sana mimi kukosea.
 

Taarifa zameibuka Marekani imetayarisha mpango wa wimbi la mashambulizi "mafupi na yenye nguvu" dhidi ya Iran katika hatua inayolenga kuvunja mkwamo katika mazungumzo na Tehran, tovuti ya habari ya Axios iliripoti.
 

Kuna uwezekano wa kizuizi cha Marekani dhidi ya bandari za Iran na usafirishaji wake kuendelezwa kwa miezi kadhaa.

 

Iran inavuruga usafiri kupitia Mlango Bahari wa Hormuz ambapo takriban thuluthu moja ya mafuta na gesi ya dunia hupita katika nyakati za kawaida.
 

Vizuizi hivyo vinaendelea kuwepo licha ya kusitishwa kwa mapigano kwa muda.
 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet