Trump hapokei simu za Infantino
Sisti Herman
August 3, 2026
Share :

Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino anapanga kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kwa nia ya kuuomba utawala wa Rais Donald Trump, kumuunga mkono anaposaka nafasi ya kuwania uongozi wa FIFA, kwa muhula mwingine.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Infantino, amejaribu mara kadhaa, bila mafanikio, kumtafuta Rais Donald Trump kwa njia ya simu, tangu mpango wake wa kuuza hisa za FIFA kukwama, siku ya Ijumaa.





