Trump kuhudhuria mazishi ya Papa Francis
Sisti Herman
April 22, 2025
Share :
Donald na Melania Trump watakuwa miongoni mwa wale watakaohudhuria mazishi ya Papa Francis huko Roma.
Rais wa Marekani amethibitisha hilo kupitia akaunti yake ya Truth Social.
Awali, Trump aliagiza bendera zote za Serikali kuu na za Majimbo zipeperushwe nusu mlingoti kwa heshima ya Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani.
“Alikuwa mtu mwema; alifanya kazi kwa bidii; aliupenda ulimwengu. Na ni heshima kufanya hivyo,” alisema.