Trump: Mwezi ni mali ya USA
Sisti Herman
September 7, 2026
Share :

"Mwezi ni Wetu," Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza katika chapisho kwenye mtandao wa Truth Social mnamo Septemba 6, akishiriki picha ya mwezi iliyowekwa maneno hayo na bendera ya Marekani.
Chapisho hilo lilikuja dakika chache baada ya Trump kushiriki picha zilizotengenezwa kwa teknolojia ya akili bandia (AI) zikionyesha sare mpya nyeusi za Kikosi cha Anga za Juu cha Marekani (US Space Force), akielezea rangi hizo kuwa ni "kijivu cha anga, nyeusi ya usiku wa manane, kijivu cha rangi ya fedha, na nyeusi ya satin."





