Try Again ahudhuria mkutano wa WFS Saudi Arabia
Eric Buyanza
December 14, 2023
Share :
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Abdallah "Try Again" amehudhuria Kilele cha mkutano wa World Football Summit (WFS) inayofanyika nchini Saudi Arabia kwa siku mbili ambayo ilifanyika Jana Desemba 12 na leo Desemba 13 katika mji wa Jeddah.
Katika mkutano huo wa World Football Summit Try Again pia amepata kozi ya FIFA Diploma in Club Management ambayo ilikuwa inatolewa na wakufunzi mbalimbali wa soka Duniani.
Pichani upande wa kulia wa Try Again yupo, Marcelo Salazar ambae ni Executive Director wa Al Nassri ya Saudia anayocheza Cristiano Ronaldo pamoja na Sadio Mane.
Upande wake wa kushoto ni Jorvan Vieira ambae ni Kocha mkubwa barani Afrika ambae alishaifundisha Wydad Casablanca, Zamalek, Etoile Sahel, timu ya taifa Morocco, Romania, Oman, Kuwait, Ismaily na FAR RABAT.