'Try Again' ajiuzulu Simba, Mo amteua tena
Sisti Herman
June 12, 2024
Share :
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Salim Abdallah “Tryagain” amejiuzulu kuendelea kuitumikia nafasi hiyo.
“Kwa maslahi mapana ya Simba kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimemwomba Mwekezaji wetu Mohamed Dewji 'Mo' arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama Mwanachama na Kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba, kwa maana hiyo natangaza kuondoka kwenye kiti” - alisema Try Again.
Masaa machache baada ya kujiuzulu Try Again, mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji alihutubia baada ya kurejea kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi na kumteua tena ‘Try Again’ kuwa mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo upande wa Mwekezaji huku akiahidi kuteua wajumbe wengine wakati ujao.