Tshisekedi amteua Judith Suminwa kuwa Waziri Mkuu Kongo
Eric Buyanza
April 2, 2024
Share :
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua waziri wa mipango Judith Suminwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.
Suminwa ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo wa waziri mkuu nchini Kongo. Uteuzi wa Suminwa unakamilisha wiki kadhaa zilizoghubikwa na hali ya sintofahamu kuhusu wadhifa huo.
Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Suminwa amesema kuwa anafahamu kuhusu jukumu kubwa linalomkabili na kuongeza kuwa atafanya kazi kuhakikisha kuwepo kwa amani na maendeleo nchini humo.