pmbet

Tshisekedi na Kagame wasaini mkataba wa amani mbele ya Trump

Eric Buyanza

December 5, 2025
Share :

Rais Donald Trump wa Marekani, amewapongeza viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, kwa ujasiri wao wa kusaini mkataba wa amani.

Mkataba huo uliotiwa saini mjini Washington unalenga kuumaliza mzozo wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Hatua hiyo kulingana na Trump itazifungua hifadhi za madini muhimu ya Kongo kwa Marekani na kampuni zake.

Kabla kusainiwa kwa mkataba huo wa amani, Trump alisema ni siku nzuri kwa bara la Afrika na dunia nzima kwani utawala wake umefanikiwa pale wengi waliposhindwa.

Hata hivyo mkataba huo umetiwa saini huku kukiwa na taarifa kwamba mapigano bado yanaendelea mashariki mwa Kongo kati ya jeshi na wanamgambo, ila Trump alipoulizwa kuhusiana na hilo na ni lini kutakaposhuhudiwa wanamgambo na wanajeshi kujiondoa kutoka eneo hilo, alisema matokeo ya mkataba huo wa amani yatakuwa ya ya haraka. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet