Tshisekedi Rais Mteule DRC
Sisti Herman
January 1, 2024
Share :
Tume Huru ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, (Ceni) imemtangaza mgombea wa kiti cha Urais, Felix Tshisekedi kuibuka kidedea kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba 20 mwaka huu kwa zaidi ya asilimia 73 ya kura zote. .
Tshisekedi alikuwa akichuana na wapinzani wake kina Moise Katumbi, Martin Fayulu na Denis Mukwege katika uchaguzi ulioghubikwa na malalamiko ya wapinzani hao.