pmbet

Tshisekedi: Ruto amevuruga mazungumzo ya Amani Congo DR

Sisti Herman

July 28, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema Rais wa Kenya, William Ruto amevuruga mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kati ya Serikali ya DRC na Makundi ya Waasi.

Akizungumza katika mjadala wa hali ya DRC ulioandaliwa na Brookings Africa Security Initiative na Africa Growth Initiative, amesema “Kuna michakato miwili. Kulikuwa na Mchakato wa Nairobi ulioendeshwa na Uhuru Kenyatta ambao kwa bahati mbaya, ulisimamiwa na Rais mpya William Ruto aliuvuruga vibaya sana”.

Inadaiwa kuwa Mei 2024, Rais Ruto akizungumza na Majarida ya Jeune Afrique na The Africa Report alisema Rwanda haipaswi kulaumiwa kama Waasi wa M23 ni raia wa DRC. Siku chache baadaye Tshisekedi aliwarudisha nyumbani Mabalozi wake nchini Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet