pmbet

Tuchel yupo na Uingereza hadi 2028

Sisti Herman

February 12, 2026
Share :

 

Thomas Tuchel amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza hadi 2028.
Mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika baada ya Kombe la Dunia la 2026, lakini sasa ataendelea kuwa kocha mkuu hadi michuano ya Euro 2028.

Tuchel, ambaye alichukua nafasi ya Gareth Southgate mwezi Oktoba 2024, amesema kuwa anafuraha na fahari kuendelea kuwa sehemu ya timu ya taifa ya Uingreza. "Ni nafasi kubwa na tutafanya kila tuwezalo kuifanya nchi ijivunie" alisema Mjerumani huyo.

Uamuzi huu unazima tetesi za kwamba Tuchel anaweza kuwa kocha mkuu wa Manchester United baada ya Kombe la Dunia.


FA wamesema kuwa mkataba huu mpya utawapa uhakika na umakini kamili kwenye Kombe la Dunia huko Marekani, Mexico na Canada.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet