pmbet

Tukiaminiwa tunaweza - Kocha Stars

Sisti Herman

January 22, 2024
Share :

Kaimu kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Suleiman Morocco baada ya timu yake jana kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Zambia amesema ni umakini kidogo ulipungua kwa wachezaji wake.

 

Hemed ameweka wazi kuwa kama wakiaminiwa kupewa kikosi hicho kukinoa wanaweza kufanya kitu kikubwa zaidi kama ambavyo wengine wanafanya wanapoaminiwa kwenye mataifa yao.

 

Hemed ameweka wazi kuwa wana nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata kama wakishindi mchezo wao dhidi ya Congo Dr.

 

“Dakika za Mwisho tukosa utulivu ndio imesababisha Zambia wafurahi kiasi fulani, nafikiri ndio mchezo, tutarudi kwenye uwanja wa mazoezi kurekebisha kile ambacho kilikuwa kinaonekana katika mechi hii”.

 

“Naamini tukienda mbele tunaendelea. Tulikuwa na mbinu nzuri, tungekuwa makini tungemaliza mechi haraka, bado nahitaji kufanya kazi zaidi, tulicheza vizuri kipindi cha kwanza, tulitengeneza nafasi nyingi”.

 

“Ni kitu cha faraja kwamba kila mchezaji anajituma, tuna machaguo mengi, kama alivyofanya Msuva na wengine wanapaswa wafanye hivyo hivyo, naamini mechi inayofuata tutakuwa na nguvu zaidi”.

 

“Tuna nafasi, mpira unazungumza katika lugha moja, tukiweza kuaminiwa tunaweza kufanya kitu kikubwa vile vile kama ambavyo wengine wanafanya”, Alisema Hemed Suleiman Kaimu kocha mkuu Taifa Stars.

 

Katika mchezo huo Stars walofunga goli lao kupitia Simon Msuva mapema kipindi cha Kwanza kabla ya Chipolopolo [Zambia] kusawazisha dakika za jioni kupitia kwa Patson Daka.

 

Chipolopolo kwenye mchezo huo walicheza wakiwa pungufu kwa takribani dakika 45 lakini haikuwatoa kwenye mchezo na zaidi waliendelea kuweka presha langoni mwa Stars.

 

Hemed Suleiman amekabidhiwa kijiti cha kuiongoza Taifa Stars katika michezo iliyosalia ya kundi F baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho Adel Amrouche kufungiwa na shirikisho la soka Afrika [CAF].

 

Tanzania imesalia na mchezo mmoja dhidi ya DR Congo ambao itaucheza kesho Jumanne ili kujua hatma yake ikoje, bado ina nafasi ya kusonga mbele kwenye kundi hili kwani inahitaji ushindi pekee kwenye mchezo ujao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet