pmbet

Tukijipanga vyema tunatoboa CAF - Ali Kamwe

Eric Buyanza

October 29, 2026
Share :

Baada ya hatua ya Makundi kuwekwa wazi Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema wakijipanga vyema katika Kundi lao B wanatoboa.

 

Kamwe amesema kucheza na timu za MC Alger, Zamalek na Club African sio ratiba rahisi, hivyo wanahitaji kujipanga vyema ili waweze kusonga mbele.

 

“Tukijipanga vyema tunaweza na mchezo wetu wa kwanza dhidi ya MC Alger ndio utatoa picha halisi ya mashindano ya msimu huu.

 

“Kauli mbiu yetu katika mashindano haya ni ile ile ya Tunanyonga na kubonda na niwaambie watu huu ni wakati wetu wa kufanya vizuri na kusonga mbele” alisema Kamwe.
 

Kamwe aliwasema watu wanaoikatia tamaa Yanga hawana shida nao, kubwa wana Wanachama na Mashabiki wanaowaunga mkono, hivyo hawana shida na wanaowabeza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet