"Tukipoteza dhidi ya TMA itakuwa habari kubwa sana"-Allan Okello.
Joyce Shedrack
April 10, 2026
Share :
Kiungo wa klabu ya Yanga Allan Okelo amesema wataenda kucheza mchezo wa TMA kama ilivyo michezo mingine kwenye ligi ili waweze kusonga mbele hatua inayofuata.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa Michuano ya FA hatua ya kumi na sita bora (16) dhidi ya TMA STARS mchezo huo utachezwa kesho kwenye uwanja wa Kmc complex majira ya 12 jioni.
Okelo amebainisha kuwa lazima wajitoe ndani dakika 90 iliwasiweze kupata presha za kupiga penati kutokana na mchezo huo kuhitaji matokeo pekee ya ushinid na siyo kuvuna alama kama ilivyo ligi kuu.





