pmbet

Tuko karibu kushinda vita dhidi ya Hamas - Netanyahu

Eric Buyanza

April 8, 2024
Share :

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake inakaribia kushinda vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

Netanyahu ameapa kuwa makubaliano hayatokuwepo hadi kundi hilo litakapowaachia mateka wote inaowashikilia. 

Akizungumza na Baraza lake la mawaziri hii jana wakati vita hivyo vikiingia mwezi wake wa sita, Netanyahu amesema Israel haiwezi kuyakubali matakwa ya Hamas. 

"Kusalimu amri mbele ya Hamas yatalifanya kundi hilo kujaribu kurudia walichokifanya Oktoba 7 kama ilivyoahidi kufanya. Hamas inadhani kuwa shinikizo kutoka nje na ndani ya Israel kutafanya tuyakubali matakwa yao. hilo halitotokea. Badala ya shinikizo kuelekezwa Israel jumuiya ya kimataifa inapaswa kuelekeza shiniko hilo kwa Hamas na hii itasaidia kuachiwa kwa mateka," alisema Benjamin Netanyahu.

Hamas ilithibitisha kwamba moja ya matakwa yake katika mazungumzo hayo ni kusitishwa kabisa mapigano mjini Gaza na wanajeshi wa Israel kuondoka huko.

Mapigano kati ya Israel na Hamas yalianza Oktoba 7 wakati wanamgambo hao walipovamia kusini mwa Israel na kusababisha mauaji ya waisraeli 1,200 nayo Israel ikaanzisha mashambulizi katika ukanda wa Gaza na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 32,000 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet