pmbet

Tuko tayari kujibu vitisho vyovyote kutoka nchi za magharibi - Putin

Eric Buyanza

June 24, 2026
Share :

Rais Vladimir Putin amesema nchi za Magharibi, zikiongozwa na jumuiya ya kujihami ya NATO, zinajiandaa kikamilifu kwa vita dhidi ya Urusi, huku zikiongeza bajeti zao za ulinzi.

 

Putin aliyasema hayo katika Ikulu ya Kremlin alipowahutubia mamia ya maafisa waliohitimu chuo cha kijeshi, akiongeza kuwa kwa sasa nchi za Magharibi zinaiunga tu mkono Ukraine, lakini kumekuwepo mazungumzo ya wazi ya nchi hizo kujiandaa kwa vita dhidi ya Urusi.

 

Putin ameendelea kuwa ili kuhalalisha uvamizi huo, mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO yanatumia madai ya uongo kuhusu uwepo wa tishio la kijeshi kutoka kwa Urusi, huku akisisitiza kuwa nchi yake iko tayari kujibu vitisho vyote vya ndani na nje.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet