pmbet

Tulijua angeondoka, lakini hatukujua ingekuwa hivi!

Eric Buyanza

May 25, 2026
Share :

Tulijua kwamba siku moja Mohamed Salah angelazimika kusema kwaheri, lakini hatukuwahi kufikiria ingekuwa na maumivu kiasi hicho kwa baadhi ya mashabiki na hata kwa yeye mwenyewe.

 

Jana Jumapili May 24 wakicheza dhidi ya Brentford F.C ilikuwa ndio mechi yake ya mwisho baada ya miaka 9 ya kuitumikia klabu hiyo kongwe.

Hakuweza kuyazuia machozi yake wakati alipokuwa anaagwa, alipiga magoti na kuubusu uwanja wa Anfield kwa mara ya mwisho. 


Wakati ambao alionekana kuguswa zaidi ni pale alipowakaribia mashabiki wa Liverpool akiwa ameambata na binti zake na uwanja mzima uliimba "You'll Never Walk Alone" kwa mara ya mwisho. 
Mohamed Salah alishindwa kuvumilia akadondokwa na machozi.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet