Tulistahili kuondolewa, tumecheza vibaya mechi zote 3 - Joshua Kimmich
Eric Buyanza
June 30, 2026
Share :
Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joshua Kimmich, amekiri wazi kuwa walistahili kutolewa.
Kauli hii ameitoa mara baada ya Ujerumani kufungwa kwa matuta 4-3 na Paraguay katika hatua ya 16 bora (Round of 32) mnamo Juni 29, 2026, kufuatia sare ya goli 1-1 katika dakika 120
"Najisikia vibaya. Hatukucheza vizuri dhidi ya mpinzani wetu yeyote. Tulicheza vibaya katika mechi zote tatu dhidi ya timu ambazo si za kiwango cha kimataifa. Huo ni ukweli. Tulistahili kuondolewa."





