Tuliyemtaka kajileta - Singida
Sisti Herman
January 10, 2024
Share :
Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup kati ya Singida FGFC dhidi ya Simba Sc, msemaji wa klabu ya Singida Fountain Gate, Hussein Massanza akitoa tahmini yake amesema mchezo wao wa nusu fainali Mapinduzi Cup dhidi ya Simba ni mechi waliyoisubiri sana.
“Tulliyemtaka kaja, kajileta, hui ndiyo mechi ya maamuzi na Simba ni timu nzuri lakini tunaisubiri kwenye mechi ya maamuzi mechi ambayo tukicheza tunatafuta kitu, utayari wa wachezaji kuelekea huo mchezo ni mkubwa sana” alisema Masanza akikaririwa na PM Sports.
Mechi hiyo itapigwa leo saa 2:15 usiku ambapo mshindi atacheza fainali dhidi ya Mlandege waliowaporomosha APR jana.