pmbet

Tumeanza safari kuwafuata Medeama, tunaomba dua zenu

Eric Buyanza

December 5, 2023
Share :

Klabu ya Yanga leo saa 10 Alfajiri imeanza safari ya kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mchezo wa raundi ya 3 wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Medeama itakayopigwa jijini Kumasi.

"Tukifika Ghana majira ya saa 5 asubuhi, tutakuwa na muda wa kupumzika jijini Accra halafu tutaunganisha safari kuelekea Kumasi ambayo ni mwendo wa dakika 45, tunaamini tutakuwa na safari nzuri kwa dua za wanachama na mashabiki wa Yanga  tutapata matokeo mazuri" alibainisha Ali Kamwe akiongea na televisheni ya mtandaoni ya klabu hiyo.
 

Wananchi wanaelekea Ghana wakiwa wa mwisho kwenye kundi D wakiwa na alama 1 tu kwenye michezo miwili dhidi ya Al Ahly na CR belouizdad.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet