"Tumechoka kumaliza msimu bila Kombe" William Saliba.
Joyce Shedrack
January 15, 2026
Share :
Beki wa klabu ya Arsenal na Timu ya Taifa ya Ufaransa William Saliba amefunguka kuwa msimu huu wanataka kushinda kila kombe kwa sababu wamechoka kumaliza msimu bila kushinda chochote.

“Kwa upande wangu, sisi ni pea bora zaidi ya walinzi wa kati Duniani lakini kwa sasa tunataka kushinda kila kombe"
“Nimechoka kumaliza msimu bila kuwa na chochote mfukoni tutatoa kila kitu, tunataka kushinda mataji.”
“Mfuko wangu ulikuwa mtupu msimu uliopita, sasa tunataka kushinda kila kitu. Kombe la Carabao, FA Cup, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu Sio rahisi lakini tunataka kuthibitisha hilo uwanjani na tutatoa kila kitu kushinda kila taji.”
“Kwa maoni yangu ndiyo, tuna ushirikiano bora zaidi duniani, lakini lazima tuthibitishe kwa kushinda mataji, kwa sababu ukisema wewe ni bora halafu hushindi chochote, hilo halina maana yoyote” Amesema Saliba.





