"Tumejipanga kuishangaza Simba na Tanzania"Msemaji wa B19.
Joyce Shedrack
March 3, 2026
Share :
Kuelekea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la TFF, uongozi wa timu ya B19 FC umepanga kuwashangaza Simba SC katika mchezo wao.
Kikosi hicho kitakwaana na Simba SC katika 32 Bora ya mashindano hayo na uongozi huo umesema umepanga kuandika historia ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza na PMTV Tanzania, Mkuu wa Idara ya Habari na MawasiliaB19, Felix Makota amesema wanawaheshimu Simba SC, lakini wamepanga kuwatoa katioa mashindano.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi katika Uwanja wa Meja Isamuhyo, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.





