Tumekubaliana tuzae watoto 8 – Billnass
Eric Buyanza
December 3, 2024
Share :
Msanii Billnass ambaye kwasasa anafanya vizuri na ngoma yake 'Magetoni', amefunguka kidogo kuhusu maisha yake ya ndani huku akitaja idadi ya watoto ambayo yeye na mke wake Nandy wamepanga kuwa nao kama mungu akiwajalia.
Haya ndiyo majibu ya Billnass wakati akijibu swali la mwandishi wa habari;
MWANDISHI: Ungependa kuzaa watoto wangapi na Nandy?
BILLNASS: Mimi napenda sana watoto na yeye anajua kabisa, tumekubaliana tuzae watoto nane alafu ndiyo atapumzika.
👉MWANASPOTI