Tumenyimwa uwanja wa mazoezi - Kocha Medeama
Sisti Herman
December 19, 2023
Share :
Kocha mkuu wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana Evans Augustin amelalamika kuwa wamenyimwa uwanja wa kufanyia mazoezi tangu wamefika hawajafanya mazoezi.
"Tangu tumekuja tumeshindwa kufanya mazoezi, tunajikuta tunafanyia mazoezi hotelini. Tumekosa uwanja wa kufanyia mazoezi sijajua ni kwanini, ila hii ni changamoto ambayo tumekutana nayo ila sijui kwanini tumekosa, zipo ishara zinazoonyesha kuwa tumenyimwa". amesema Kocha Mkuu wa Medeama SC, Evans Augustin kwenye mkutano na waandishi wa habari
Medeama itacheza na Yanga kesho kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.