pmbet

"Tumeshamaliza yetu wamebaki wao"

Eric Buyanza

December 8, 2023
Share :

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ambaye pia anawakilisha ubalozi wa Tanzania nchini Morocco, Sekela Mwambegele amesema maandalizi yaliyohitajika kufanywa na ubalozi ambao ni wenyeji wa Simba nchini Morocco yameenda vyema hadi sasa kazi imebaki kwa Simba ufanya kila kitu kwa uwezo wao.
 

"Sisi kama ubalozi tumeshiriki katika zoezi la kuwapokea na kuhakikisha "Logistic" muhimu zipo vizuri kabisa usalama wa wachezaji, usafiri, malazi na kama unavyoona wanaendelea na maandalizi ya mchezo" amesema Sekela akiongea na idara ya habari ya Simba.
 

Simba ambao wako nafasi 3 kwenye kundi B lenye timu za Wydad AC, Jwaneng' Galaxy  pamoja na Asec Mimosas watacheza kesho usiku dhidi ya Wydad Athlethic Club jijini Marrakech kwenye mchezo wa raundi ya 3 wa ligi ya mabingwa barani Afrika 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet