pmbet

"Tumetoka mapema kwasababu hatukuwa makini" - Kudus

Sisti Herman

January 23, 2024
Share :

Nyota wa klabu ya Westham United na timu ya Taifa ya Ghana Mohamed Kudus ameonyesha kusikitishwa baada ya kutolewa kwa timu yake ya Taifa kwenye fainali za mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Ivory Coast licha ya uwezo mkubwa aliouonyesha.

 

Kudus amesema walipaswa kupata zaidi ya kile walichokipata kwani walifanya kila kitu ili kupata matokeo lakini mwisho wa siku mambo yameenda mlama kwa upande wao.

 

“Nimeumizwa sana, tulikuwa tunahitaji zaidi ushindi lakini haijatokea”.

 

“Ni huzuni kubwa sana kwetu”, Alisema Mohamed Kudus.

 

Ghana walishindwa kuyalinda magoli mawili ambayo waliyapata kwenye mchezo wao dhidi ya Msumbiji hapo jana na dakika za mwisho wakasawazishiwa na hivi kuondoshwa kwenye michuano hiyo.

 

“Tulipoteza mchezo kwa kukosa umakini kwenye dakika za mwisho, kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Misri”.

 

Kudus anaamini Ghana wameonyesha uwezo mkubwa sana kwenye michuano hii inayoendelea hapa nchini Ivory Coast.

 

“Tumeonyesha uwezo mkubwa sana hapa lakini kukosa umakini mwishoni umetugharimu”, Alimaliza Mohamed Kudus.

 

Mohamed Kudus alitajwa kuwa nyota wa mchezo huo dhidi ya msumbiji hapo jana licha ya timu yake kuondoshwa na hii inakuwa mechi yake ya pili mfululizo kutajwa kuwa nyota wa mchezo.

 

Mashabiki wengi wa soka nchini Ghana wanatoa lawama zao kwa kocha Chris Hughton kwa kushindwa kukiongoza vyema kikosi chake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet