Tumewaangusha wabrazil wote - Casemiro
Eric Buyanza
July 6, 2026
Share :

Kiungo wa Brazil, Casemiro, alibubujikwa na machozi baada ya timu yake kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alizungumza hayo baada ya Brazil kufungwa mabao 2-1 na Norway katika hatua ya 16 bora siku ya Jumapili.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alikiri kuwa kikosi cha Carlo Ancelotti kiliwaangusha Wabrazil wote, akiongeza kuwa watakumbukwa kama kizazi ambacho hakikutwaa Kombe la Dunia.
"Ni ngumu kuamini....kwasasa ninataka tu kuwa na familia yangu. Tulijitahidi kadri ya uwezo wetu, lakini tumepoteza ndoto yetu... tumewaangusha Wabrazil wote"
"Siku zote tutakuwa kizazi ambacho hakikutwaa Kombe la Dunia" alisema Casemir kwa uchungu mkubwa.





