pmbet

"Tumewatoa Misri, Morocco walikuwa wepesi, hatujaipania Tanzania" - Mayele

Sisti Herman

January 29, 2024
Share :

Baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Misri kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo, mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Congo DR Fiston Mayele amesema kwao mechi dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco ilikuwa rahisi kulinganisha na Misri ambayo iliwapa wakati mgumu hadi kufanikiwa kuitoa kwenye mashindano ya AFCON usiku wa kuamkia leo.

Akiongea kwa furaha baada ya kuitoa Misri kwa penati, Mayele amenukuliwa akisema "Jamani siwezi kujisahau hii ndio Congo, hakuna Mtu ambaye alikua anategemea kama sisi tungemtoa Misri na tumemtoa leo kesho anarudi nyumbani, so kusema sisi tulipania mechi ya Tanzania tunapania vipi bwana ? mbona Morocco wepesi, Misri wana Timu kubwa wana Timu nzuri sana wametuhangaisha"

"Ndugu zangu Watanzania mimi nawapenda sana, ndio Nchi yangu ya pili... nadhani nusu ya Watanzania walikua nyuma yetu, leo ni siku kubwa kwetu siku ya furaha, sina maneno wallah, wallah sina maneno" 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet