"Tumonyesha ukubwa wetu" - Feitoto
Sisti Herman
March 18, 2024
Share :
Kiungo wa klabu ya Azam Feisal Salum “Feitoto”baada ya ushindi wao wa 2-1 huku yeye akifunga goli dhidi ya Yanga jana amesema kuwa ushindi huo dhidi ya timu yake ya zamani ni sehemu ya kuonyesha ukubwa na ubora wao kwasasa.
“Nyakati zote zilikuwa ngumu kwasababu Yanga wana timu nzuri, timu bora, wana wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa, tumeonyeshana ukubwa” alibainisha Feisal akiongea na PM Sports.
“Nawaheshimu sana Yanga, ni timu ambayo imenitoa hatua moja kwenda nyingine, kwahiyo isingekua vizuri mimi nikashangilia” aliongeza Feisal akiongelea kuhusu kutoshangilia baada ya kufunga.