Tuna mashaka na nia ya Marekani - Iran
Eric Buyanza
April 19, 2025
Share :
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema anatilia shaka nia ya Marekani, siku moja kabda ya kufanyika mjini Roma kwa duru ya pili ya mazungumzo kati ya nchi hizo mbili kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.
Araghchi ameyasema hayo siku ya Ijumaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Moscow akiwa na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov, na kusisitiza kuwa licha ya mashaka makubwa juu ya nia ya Marekani, watashiriki kwa vyovyote vile mazungumzo hayo ya leo Jumamosi.
Hata hivyo Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran amesema anaamini kuwa makubaliano ya nyuklia na Marekani yanawezekana kwa msaada wa Urusi huku Lavrov akisema Moscow iko tayari kutoa mchango wake kuwezesha mpango huo.
DW