pmbet

Tunaenda sauzi kuanza kazi upya – Kapombe

Eric Buyanza

April 23, 2025
Share :

Nahodha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi, Shomari Kapombe, amesema mpango wao ni kwenda South Africa kuanza kazi upya ya kuwakabili Stellenbosch FC wakiwa wamesahau bao moja walilopata nyumbani.

Stellenbosch itaikaribisha Simba SC katika mechi ya marudiano ya hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, Durban nchini Afrika Kusini.

Simba SC ilipata shindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumapili ilivopita hivyo inahitaji sare ya aina yoyote ili kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo inayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Kapombe, anasema wataingia uwanjani kwenye mechi ya marudiano kama vile hawana chochote mkononi ili iwasaidie kuongeza juhudi ya kupambana zaidi.

NIPASHE 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet