"Tunahitaji jamii inayoweza kuhoji"
Eric Buyanza
December 10, 2023
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan amesema taifa linapaswa kuwa na jamii yenye ujasiri inayoweza kuhoji watu wanaojipatia mali zisizo na maelezo nazo.
Rais amesema hayo jana alipohutubia maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.
“Jamii inayochukia rushwa kila mahali, jamii inayoweza kujituma kufanya kazi bila kusukumwa, inayopinga uchakachuji wa mazao kama pamba na korosho kuongezwa mawe na jamii inayolaani ukwepaji wa kodi.”amesema Rais Samia.