pmbet

"Tunahitaji kushinda nyingi kwa Ahly ili tufuzu" - Benchikha

Sisti Herman

March 29, 2024
Share :

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Abdelhak Benchikha amesema wanahitaji kumaliza kwa idadi kubwa ya magoli nyumbani mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ili kurahisisha mazingira ya kufuzu nusu fainali.

"Kila timu inapenda inapokuwa katika uwanja wake wa nyumbani ipate magoli mengi na sisi tunahitaji kufanya hivyo lakini itategemeana na mchezo utakavyokuwa kwetu na kwa wenzetu pia." alisema Abdelhak Benchikha

Simba watakuwa wenyeji wa Ahly leo kuanzia saa 3 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Temeke Dar es Salaam.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet