Tunahitaji kuwa na umoja - Himid
Sisti Herman
January 3, 2024
Share :
Mchezaji mwandamizi wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Himid Mao amewaomba Watanzania kuwa na umoja na kuiunga mkono timu ya Taifa wakati huu ikijiandaa na michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
“Tunahitaji kuwa pamoja Watanzania tunahitajiana, sisi wachezaji na timu tunahitaji Watanzania wenzetu, tunahitaji sana sapoti yao kwahiyo umoja wetu ni kitu muhimu sana, tunaweza kufanya kitu kikubwa zaidi tukiwa wamoja” alisema Himid kwenye mahojiano na afisa habari wa shirikisho la soka nchini Clifford Mario Ndimbo kupitia TFF Tv.
Himid ameyasema hayo mara baada ya mazoezi ya kwanza ya Stars kwenye kambi fupi ya kujiandaa AFCON iliyowekwa nchini Misri kabla hawajaunga kwenye nchi mwenyeji wa mwashindano Ivory Coast.
Kuhusu mazoezi Himid aliongoza “Mazoezi yamekuwa mazuri, wachezaji wana ari kubwa zaidi na ukizingatiaa leo ndiyo siku ya kwanza naamini tutakuwa chanya zaidi hasa wachezaji wengine wakiongezeka tutakuwa vizuri zaidi”.
Stars ipo kundi F lenye timu za mataifa ya Morocco, Zambia na Congo DR na itacheza mechi zake za hatua ya makundi kwenye uwanja wa Laurent Pokou kwenye mji wa San Pedro.