Tunakwenda kupambana kufa na kupona Algeria - Mzamiru
Eric Buyanza
December 3, 2024
Share :
Wachezaji wa Simba, wamesema watakwenda kupigana kufa na kupona ili kupata ushindi au hata sare kwenye mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho, hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine ya Algeria.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mchezaji mkongwe wa timu hiyo, Mzamiru Yassin, amesema;
"Mechi ni ngumu, si nyepesi kama watu wanavyofikiria, sisi wengine ni wazoefu kwenye michuano hii, tunajua hilo, kinachotuaminisha hivyo ni kwamba mpinzani wetu tunaekwenda kucheza naye ametoka kushinda ugenini, akiifunga timu kubwa kama CS Sfaxien ya Tunisia ambayo kwenye kundi letu ndiyo ina historia nzuri ya michuano hii kuliko timu yoyote.
"Kama hao jamaa Watunisia wamefungwa kwao, ina maana si timu ya kubeza, ndiyo maana tumekomaa kwenye mazoezi," alisema mchezaji huyo.
NIPASHE