"Tunamtakia kila la kheri Mbappe" - Kocha PSG
Sisti Herman
March 11, 2024
Share :
Kocha mkuu wa PSG Mhispaniola Luis Enrique amefunguka rasmi kuhusu suala la uhamisho wa mshambuliaji nyota wa timu hiyo Mfaransa Kylian Mbappe huku akithibitisha kuwa ni kweli hatokuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao.
"Namtakia kheri Mbappe huko aendako, ni mchezaji bora lakini pia ni mtu mwenye utu, kiukweli tunamtakia kila lililo kheri" - Luis Enrique, kocha wa PSG
Mbappe anahusishwa kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa mkataba wake na PSG.