pmbet

"Tunaonewa" licha ya kutinga fainali Guardiola alalamika ratiba

Sisti Herman

April 21, 2024
Share :

Baada ya klabu ya Manchester City kutinga fainali ya kombe la FA England kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika dimba la Wembley kwenye nusu fainali, kocha wa timu hiyo Pep Guardiola amesema kuwa upangaji wa ratiba kwenye michuano mbalimbali msimu huu unawaonea.

"Hatukutakiwa kucheza Jumamosi wakati tulikuwa na mechi Jumanne, Man Utd na Chelsea hawachezi Uefa wala Europa na hawachezi katikati ya wiki" alisema Guardiola

Manchester City imetangulia nusu fainali kwa bao la pekee la Bernado Silva na sasa inamsubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Coventry dhidi ya Manchester United itakayopigwa kesho katika dimba la Wembley.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet