"Tunataka kutimiza ndoto za wachezaji wanaotaka kujiunga Barca" -Laporta.
Joyce Shedrack
June 30, 2026
Share :
Rais wa Barcelona Joan Laporta amesema wanaimani wataweza kutimiza ndoto za wachezaji wanaotaka kujiunga na Barcelona ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji wa Atletico Madrid Julian Alvarez kusema anataka kutimiza ndoto yake alipoulizwa kuhusu hatma yake kuelekea msimu ujao.

"Tunataka kutimiza ndoto za wachezaji,Tunatumaini tunaweza kutimiza ndoto za wachezaji wanaotaka kujiunga na Barça."
"Ni wazi kwamba ndoto zinaweza kuwa kweli. Ukifanya kazi kwa bidii na kupigania ndoto zako, zinaweza kutimia. Ninafurahi kuona kuna wachezaji wengi wanaotaka kujiunga na Barça, na jambo hilo linatupa fahari kubwa."Amesema Joan Laporta.





