"Tunawasiliana na Ronaldo ananisaidiaga sana" - Mbappe
Sisti Herman
July 5, 2024
Share :
Nahodha wa timu ya Taifa Ufaransa Kylian Mbappe amesema huwa anawasiliana mara kwa mara na nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo na amekuwa akimsaidia mara kwa mara.
"Bado tunawasiliana, Cristiano amekuwa msaada mkubwa kwangu, anafuatilia kila kinachoendelea kwenye maisha yangu na amekuwa akinipa baadhi ya mbinu na kila mtu anajua ni namna gani namkubali" alisema Mbappe.
"Tangu nipo kijana mdogo nilikuwa na ndoto kubwa ili nije kuwa kama Cristiano Ronaldo" alimaliza Mbappe.
Mbappe ambaye anamuangalia Ronaldo kama 'Role Model' wake ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa robo fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya utakaowakutanisha mataifa hayo mawili.
Mbappe ambaye pia ni nyota mpya wa klabu ya Real Madrid amekuwa akijitahidi kufuata nyayo za Ronaldo ambaye ni gwiji wa Real Madrid.