Tunaweza kuirejesha Lebanon kwenye zama za mawe - Yoav
Eric Buyanza
June 27, 2024
Share :
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema taifa lake halitaki vita na Lebanon, ingawa ameonya kuwa hawatasita kuishambulia vibaya ikiwa juhudi za kidiplomasia zitashindwa.
Gallant amewaambia waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Washington kwamba hawako tayari kwa vita, ingawa wamejiandaa kwa chochote kinachoweza kutokea.
Amesema Hezbollah wanatambua vizuri kwamba Israel inaweza kuleta uharibifu mkubwa huko Lebanon, kama watapigana vita.
Ameongeza kuwa jeshi la Israel lina na uwezo wa kuirejesha Lebanon kwenye "zama za mawe", katika vita dhidi ya kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.
DW imeripoti Maelfu ya watu kaskazini mwa Israel na kusini mwa Lebanon wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya Hezbollah na jeshi la Israel.