pmbet

Tunisia yamtambulisha kocha Herve Renard kwa ajili ya Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

June 16, 2026
Share :

Kocha mwenye uzoefu mkubwa, Hervé Renard, ameteuliwa kwa dharura kuiongoza timu ya taifa ya Tunisia katika Kombe la Dunia la FIFA 2026, baada ya shirikisho la soka la nchi hiyo kumfuta kazi kocha Sabri Lamouchi kufuatia mwanzo mbaya wa mashindano.

Tunisia names Hervé Renard as new FIFA World Cup coach after sudden axing  of Sabri Lamouchi - ABC News

Baada ya Tunisia kufungwa mabao 5-1 na Sweden katika mechi yao ya kwanza, Shirikisho la Soka la Tunisia (TFF) lilichukua uamuzi wa haraka wa kumtimua Lamouchi, ambaye alikuwa ameajiriwa mwezi Januari kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.

 

Renard mwenye umri wa miaka 57 sasa amesaini mkataba wa muda mfupi wa kuinoa Tunisia hadi mwisho wa Kombe la Dunia.

 

Kocha huyo ana historia kubwa katika soka la kimataifa aliifikisha Morocco Kombe la Dunia 2018, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki baada ya miaka 20.Aliiongoza Saudi Arabia kuifunga Argentina kwa mshangao mkubwa katika Kombe la Dunia 2022.

 

Awali, Renard alikuwa anatarajiwa kuiongoza Saudi Arabia katika Kombe la Dunia 2026 katika kipindi chake cha pili akiwa kocha wa timu hiyo, lakini alifutwa kazi mwezi Aprili, miezi miwili tu kabla ya mashindano kuanza. Saudi Arabia ilianza kampeni yake kwa sare ya 1-1 dhidi ya Uruguay mjini Miami.

 

Tunisia sasa inatumaini kuwa uzoefu mkubwa wa Renard katika mashindano makubwa unaweza kuisaidia kurejea kwenye njia ya ushindani baada ya kipigo kizito katika mechi ya ufunguzi.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet