Tupo tayari kujilinda saa 24 kwa wiki dhidi ya Iran.
Joyce Shedrack
July 25, 2026
Share :
Kauli hii imekuja baada ya Iran kutishia kulenga kambi ya Jeshi la Anga la Uingereza (RAF) inayotumiwa na Marekani.

Iran imeishutumu serikali ya Uingereza kwa kile ilichokiita "ushiriki katika uchokozi na uhalifu wa kivita", ikidai kuwa imeiruhusu Marekani kutumia kambi zake kufanya mashambulizi.
Kwa upande wake, Uingereza imesisitiza kuwa haijashiriki katika mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya Iran, lakini imeruhusu Marekani kutumia baadhi ya vituo vya kijeshi vinavyohifadhi wanajeshi wa Marekani kwa kile kinachoelezwa kuwa operesheni za kujihami.





