"Tusimchague mtu kwa kuangalia dini wala kabila"RC Makonda.
Joyce Shedrack
June 7, 2025
Share :
Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amewataka wananchi wa Mkoa huo kuchagua viongozi sahihi watakaoweza kushughulikia changamoto zao bila kuangalia dini, kabila wala sura.
" uchaguzi, hatumchagui mtu kwa dini yake, kabila lake wala sura yake, yapo mambo yanayotusibu yanayopelekea kwa pamoja tuweke sauti yetu kwenye kura ya kwamba huyu tukimpa nafasi atatupa majawabu". Amesema Mhe. Makonda.
Hata hivyo amehimiza viongozi wote kwenye mkoa huo kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao hasa katika kipindi hicho cha uchaguzi