"Tutaendelea kuwaunga mkono Yanga" - Rais Samia
Eric Buyanza
April 6, 2024
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa jinsi ilivyopambana kulinda heshima ya taifa hapo jana na kuahidi kuiunga mkono timu hiyo baada ya kuonesha mchezo mzuri katika mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) Rais Samia ameandika;
"Mmeonesha kiu na juhudi ya kuiletea heshima nchi yetu hadi kufikia hatua hii. Tunatarajia makubwa zaidi kutoka kwenu kwenye mashindano haya (Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika) msimu ujao. Tutaendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha." amesema mama Samia