pmbet

Tutaifunga 'Bafana Bafana' bila kwenda kwenye matuta - Chukwueze

Eric Buyanza

February 6, 2024
Share :

Winga wa Nigeria, Samuel Chukwueze amesema Nigeria itaifunga Afrika Kusini bila kwenda kwenye mikwaju ya penalti timu hizo zitakapokutana katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023, AFCON, Jumatano hii. 

Nyota huyo wa AC Milan pia alitupilia mbali dhana kwamba mlinda mlango wa Bafana Bafana, Ronwen Williams ni mtaalamu wa kuokoa penalti.

Kumbuka kwamba Williams aliweka jina lake kwenye vitabu vya historia kama kipa wa kwanza kuokoa penalti nne kwenye game moja ya AFCON moja, wakati Afrika Kusini ilipoifunga Cape Verde 2-1 kwa mikwaju ya penalti katika robo fainali na kuandaa mechi ya nusu fainali na Nigeria. 

"Penati ni mchezo wa bahati, mtu yeyote anaweza kukosa, Sisemi kuwa yeye si kipa mzuri, ni kipa mzuri, lakini jambo la muhimu zaidi ni sisi kushinda ndani ya dakika 90 au 120. Tutashinda bila kwenda kwenye penalti." alijigamba Chukwueze.

"Sio kwamba tunawaogopa kwenye penalti!..hapana .....lakini tutakuwa salama zaidi tukifanya hivyo. Tumekuwa tukitazama klipu zao, ni wazuri kwa kiwango chao, lakini tutajaribu tuwezavyo na kushinda." alimalizia

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet