"Tutajitoa kadiri ya uwezo wetu" - Benchikha
Sisti Herman
February 23, 2024
Share :
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Abdelhak Benchikha amesema wanaenda kucheza mchezo mgumu na muhimu dhidi ya Asec Mimosas kwenye mchezo wa raundi ya 5 ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ambao kwa vyoyote vile wana uhitaji wa alama tatu ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano.
“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, tunahitaji kushinda ili tuweze kufuzu robo fainali, malengo yetu ni kupata alama tatu, Tutajitoa kadri ya uwezo wetu” maneno ya Kocha wa Simba SC, Abdelhak Benchikha akizungumzia mchezo wa kesho Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), dhidi ya wenyeji wao Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Mechi itapigwa saa 4:00 usiku na itakuwa ikitangazwa kupitia channel yetu ya Youtube ya PMTV.